Header Ads

ad

RSA walivyomsindikiza balozi Damasi Anthony katika makazi yake ya milele, jijini Dar

Marehemu Damasi Anthony, enzi za uhai wake, akiwa mwanafunzi wa UoI

Hatimaye mwili wa aliyekuwa balozi wa usalama barabarani (RSA), Damas Anthony Dogani, aliyefariki katikati ya wiki, Ijumaa hii, umepumzishwa katika makazi yake ya milele Ijumaa ya leo, katika ibada ambayo ilihudhuriwa na waliokuwa mabalozi wenzake na marehemu, waishio jijini Dar. 

Damas, ambaye pia alikuwa msaidizi wa kiongozi wa mtandao huo kwa mkoa wa Iringa, alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi, akiwa nyumbani kwao jijini Dar, takriban wiki mbili tu kabla ya kushiriki mahafali ya kuhitimu digrii yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Iringa (UoI) zamani Tumaini. 

Licha ya kufariki akiwa na umri mdogo, marehemu alishaacha "legacy" zake kutokana na aina ya maisha aliyokuwa akiishi katika maeneo mbalimbali alikoweza kupita wakati wa kujipatia elimu au kushiriki kazi za kijamii. 

Atakumbukwa kama mmoja wa mabalozi waliokuwa wako mstari wa mbele katika kuelimisha jamii kuhusu haki na wajibu wao wakati wa safari, akiamini kuwa hiyo ndio ilikuwa njia sahihi kabisa ya kupunguza wimbi la ajali nchini, kama lilivyo lengo na kauli mbiu ya RSA. 

Alikuwa kijana mcheshi, mwenye heshima na hekima, aliyependa kujifunza kila kitu, kila siku na kwa mtu yeyote yule. 

Naam, Dunia ilimpenda sana kijana huyu, lakini Muumba wetu kampenda zaidi. Kwa tunaoamini kwamba Mungu hawezi kukuchukua hadi lengo au kazi aliyokutuma duniani uje kuifanya, iwe imetimia, tunaamini kwamba, alitimiza wajibu wake ipasavyo, na hivyo atakwenda kupewa mapumziko mema mbele ya mola wetu. 

Pichani ni baadhi ya picha mbalimbali zikionyesha namna RSA walivyoshiriki msiba wa balozi mwenzao.











No comments