Header Ads

ad

Ufunguzi jengo jipya kanisa la Elshadai Temple wafana

LEO Kanisa hiyo la Elshadai Temple Internatiol lililopo eneo la Basiaya ,Boko Beach Dar Es Salaam, linaloongozwa na Nabii Kanali Mstaafu ,Bruno Kinunda,umefanyika Leo kanisani hapo nakuudhuliwa na Mamia ya waumini na marafiki wa Kanisa Hilo.

Uzinduzi wa jengo Hilo linakadiliwa Kubeba jumla ya waumini 200 limejengwa kwa michango ya waumini wa Kanisa Hilo ambapo Nabii Kinunda alisema wanawake ndiyo walioongoza kutoa michango Mimi ya Ujenzi wa Kanisa Hilo ambalo lipo Katika Hatua za mwisho za kukamilika kwa Ujenzi huo.

Nabii Kinunda alisema Kanisa Hilo ilianzishwa Miaka 14 iliyopita na kwamba kadri siku zinavyozidi kusonga Mbele waumini wamezidi kuongezeka hivyo kusababisha Kanisa walilokuwa wakilitumia awali kulivunja mapema wiki hii na Leo kuingia Katika Kanisa Hilo jipya nakuanza kulitumia.

Aidha ufunguzi wa Kanisa Hilo ambalo Leo ulikuwa ni kwaajili ya waumini wa Kanisa Hilo ambalo ndiyo wajenzi wa Kanisa Hilo ulitanguliwa na maandamano nje ya Viwanja Vya Kanisa Hilo yaliyoongozwa na Nabii Kinunda na Mchungaji Kiongozi Ambaye ni Mkewe ambapo walisimama nje ya jengo Hilo jipya wakayabariki Maji ambayo Nabii Kinunda akiongozwa wachungaji wasaidizi akiingia na Maji hayo NA Kisha kayamwaga ndani ya Kanisa Hilo ikiwa ni Ishara ya kulibariki Kanisa na kuzifungua ambapo ibada ya Leo ikiendeshwa ndani ya jengo Hilo jipya na somo la Leo lilisema ( HEKALU JIPYA KANISA LA ELSHADAI ).

Kanisa Hilo ambalo bado halijawekewa umeme ambapo Nabii Kinunda alisema jumla ya Shilingi Miliioni tano zinaitaji la kwaajili ya kuingiza umeme ndani ya Kanisa Hilo ,ndipo baadhi ya waumini walijitokeza kuchangia ambapo Jumla ya Sh.1.35 Milioni zilichwanga hapo hapo kanisani na zinatolewa NA jumla ya sh milioni 3.35 baadhi ya waumini waliaidi Kuzitoa ili ziweze kusaidia Kufuta umeme Kanisa hapo.

No comments